FM Academia, New Msasani Club

Nyoshi el Saadat na Mwamba ambae pia ni msanii muigizaji wa filamu



Kila Jumapili kuanzia kumi na mbili jioni, New Msasani Club huwa panatawaliwa na muziki mzito wa FM Academia. Nyoshi akiwa analiongoza kundi zima huleta burudani tosha ya kuimba na kucheza bila kuchoka na kwa kweli ni raha tupu. Nimekutana na dada mmoja ambaye kwa usiemjua utadhani bado ni msichana mdogona alikuwepo hapo na wanamuziki wa FM, huyu namkumbuka aliwahi kuwa na ukaribu huo huo na wanamuziki wa TANCUT , baadae nikamkuta na wanamuziki wa Vijana Jazz miaka hiyo mwishoni mwa themanini, leo nimemkuta na wanamuziki wa FM Academia kweli huyu ni mpenzi wa muziki

Comments