Thursday, July 7, 2011

What next in the Modern Taarab journey?

Asha Ramadhan aka Isha Mashauzi


Isha performing a rare thing in Taarab dancing
Yesterday I attended a unique taarab performance by Asha Ramadhan better known as Isha Mashauzi a controvesial Taaarab artiste who has decided to launch her own group Isha Mashauzi Classic. Singing mostly her own compositions including a song composed by her friend which talks about her recently broken marriage, the show was great she is a great singer no doubt. But Aisha has brought more controversy to taarab music, as it is now a lot of staunch, Taarab Asilia(Traditional Taarab) believers,  say the  so called 'Modern Taarab is not even Taarab at all', Aisha has opened a new door by dancing to the steps of her dancers while performing  a new development in Taarab

Isha Mashauzi afungua ukurasa mpya katika Modern Taarab

Isha Mashauzi ni mwanamuziki wa Taarab ambaye  atakumbukwa na wana historia wa muziki kwa mambo ambayo inawezekana hata yeye hajajua ukubwa wake. Kwanza Isha anatokea Mkoa wa Mara, mkoa huu hauonekani kabisa kama unaweza kuwa na uhusiano na muziki wa Taarabu, Isha amekwisha tunga mpaka wimbo wa kusisitiza hilo wimbo huo unajulikana kama  Isha Mtoto wa Musoma. Mavazi ya Isha yamekuwa yakileta mazungumzo katika jamii ya wapenzi wa Taarabu, na sasa ameenda mbale zaidi, katika Taarab hii ambayo wahusika huiita modern Taarab, na wapinzani wake wanasema hii sitaarabu kabisa, pamoja na kuweko na vijana wacheza show katika kundi lake, kwa mara ya kwanza tunamuona mwimbaji wa muziki huu nae akijiunga na wacheza show na kucheza nao step zao. Isha kafungua ukarasa mpya katika muziki huu

Onja Makumbele 'live'

Onja Mkumbele 'live' jana tu pale Mzalendo Millenium Tower na kila Jumatano raha hizi. Hapo yupo Tchimanga assossa na Kasongo Mpinda.


Wazee wa mjini

Assossa na Kasongo

King Kiki


Kasongo Mpinda Clayton

Ben

Tchimanga

Kabeya BaduKila Jumatano katika ukumbi wa Mzalendo, Millenium Tower wanamuziki wa zamani, wengi wao wakiwa wa asili ya Kongo wamekuwa wakiporomosha muziki wa enzi hizoooo.Miamba kama King Kiki, Tchimanga Assossa, Kasongo Mpinda huporomosha muziki hapo, vibao kama Safari yetu Mbeya(Maquis), Kibela(MK Group), nyimbo mbalimbali za Safari Sound, Kasheba Group, Zaita Muzika na bendi nyingine nyingi husikika hapo ni burudani kwa wapenzi wa muziki wa enzi hizo

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...