Skip to main content

Posts

Showing posts from April 7, 2017

MPIGA BASS GUITAR WA TOT AFARIKI BAADA YA AJALI YA PIKIPIKI

Samwel Mshana maarufu kama Mshana Bass, aliyekuwa mpiga gitaa la bezi katika kundi la TOT  amefariki dunia leo alfajiri. Samwel alikuwa amelazwa hospitali baada ya ajali, ambapo pikipiki aliyokuwa akiendesha iligongana na bajaji maeneo ya Mwananyamala Komakoma. Kifo chake kimekuwa cha ghafla na kushangaza kwa kuwa kwanza ajali haikutokea kwenye mwendo kasi na baada ya ajali hakuonekana kuwa na majeraha yoyote makubwa, na hata siku ambazo rafiki zake walikuwa wakimtembelea hospitali hakuonyesha dalili kuwa ni jambo kubwa. Kazi ya Mungu haina makosa. Mungu amlaze pema SAMWEL  MSHANA

MWANAMUZIKI UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA FETE DE LA MUSIQUE?

Haya tena wanamuziki wenzangu tamasha la FĂȘte de la Musique linawakaribisha wanamuziki wa kila aina kuomba kushiriki katika msimu wa sita wa tamasha litakalofanyika tarehe 17 mwezi juni 2017 Johannesburg, South Africa. Mwisho wa kupelka maombi ni Ijumaa tarehe 28 April 2017.
Namna ya kuomba
Wasanii wanaotaka kushiriki wapeleke maombi yao yakiambatana na :
·Maelezo ya historia ya msanii (Artist biography)
·Picha (Photo)
Maelezo ya kiufundi ya vifaa utavyotumia jukwaani (Technical rider)Nakala ya muziki wako (Sound clips)VideosMaelezo yako yatakayoweza kutumika katika matangazo (Press kit)
Maombi yote yanaweza kutumwa kupitia fetedelamusiquejoburg@gmail.com wakati fomu za maombi zinapatikana  here.
FĂȘte de la Musique ni tamasha ambalo linaweza kuhudhuriwa na familia nzima bila kujali rika, nia yake ikiwa ni kufurahia muziki wa’live’. Pia ni mahala ambapo wasanii kutoka nchi mbalimbali wanaweza kukutana.
Kwa kuwa kuna maelfu ya wapenzi wa muziki hukutana hapa katika tukio hilo la …