MWANAMUZIKI UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA FETE DE LA MUSIQUE?


Haya tena wanamuziki wenzangu tamasha la Fête de la Musique linawakaribisha wanamuziki wa kila aina kuomba kushiriki katika msimu wa sita wa tamasha litakalofanyika tarehe 17 mwezi juni 2017 Johannesburg, South Africa. Mwisho wa kupelka maombi ni Ijumaa tarehe 28 April 2017.

Namna ya kuomba

Wasanii wanaotaka kushiriki wapeleke maombi yao yakiambatana na :

·       Maelezo ya historia ya msanii (Artist biography)

·       Picha (Photo)

  • Maelezo ya kiufundi ya vifaa utavyotumia jukwaani (Technical rider)
  • Nakala ya muziki wako (Sound clips)
  • Videos
  • Maelezo yako yatakayoweza kutumika katika matangazo (Press kit)

Maombi yote yanaweza kutumwa kupitia fetedelamusiquejoburg@gmail.com wakati fomu za maombi zinapatikana  here.

Fête de la Musique ni tamasha ambalo linaweza kuhudhuriwa na familia nzima bila kujali rika, nia yake ikiwa ni kufurahia muziki wa’live’. Pia ni mahala ambapo wasanii kutoka nchi mbalimbali wanaweza kukutana.

Kwa kuwa kuna maelfu ya wapenzi wa muziki hukutana hapa katika tukio hilo la mara moja kwa mwaka, wanamuziki maarufu na wasio maarufu hupanda jukwaa moja. Tamasha lipo kwa hisani ya Alliance Francaise Johannesburg na French Institute of South Africa, wakishirikiana na Bassline Live kwa ufadhili wa Total.

Mwaka  2016, Fête de la Musique iliwakusanya karibu watu 8 000 katika mji wa Newtown, Johannesburg. Baadhi ya wasanii walioshiriki walikuwa Vaudou Game (France), Blk Jks (South Africa), Les Fantastiques (DRC), Jess & Crabbe (France), Bombshelter Beast (South Africa), Mapumba Cilombo (DRC), Morayks (Lesotho), Zanmari Baré (Reunion Island) na wengine wengi.

Comments