Skip to main content

Posts

Showing posts from July 12, 2011

Mama wa Ng'aring'ari huyooooooo

Uongozi wa juu wa Clouds Entertainment ulikuwa sambamba

Kama kawaida yao TANESCO walikata umeme ikawa ni  muda wa kutia stori, Joseph Kusaga, Ruge Mutahaba, top management ya Clouds ambao ndio wafadhili wa shughuli yote ya recording na onyesho la kundi hili tarehe 22 July pale Salender Bridge,walichukua muda wao na kuwepo katika eneo la studio


Clouds TV walikuwepo studio kuweka kumbukumbu ya kila kitu

Bendi ya Wakongwe yaingia studio

Ikiwa chini ya udhamini wa Clouds Radio na TV, bendi ya wakongwe imeingia studio kurekodi nyimbo tatu. Kuanzia Jumatatu wanamuziki hawa wamekuwa Metro Studio chini ya fundi mitambo Allan Mapigo aka Ndimu wakirekodi nyimbo hizo, 1, Miaka 50 ya Uhuru 2. Kilimo kwanza 3.Tanzania Yetu Nchi ya furaha
FM Academia yapata msiba mzito

Bendi ya FM Academia imepata msiba mkubwa baada ya kufiwa na meneja waoBonny Kasyanju ambaye aliyejulikana kwa wengi kama Uncle Bonny. Bonny ambaye mara nyingi alikuwa mlangoni katika maonyesho ya FM Academia amezikwa katika makaburi ya Kinondoni. Bonny alikuwa nguzo muhimu katika shughuli za FM Academia Mungu amlaze pema peponi. Ameni