Friday, June 3, 2011

Lady JD and The Machozi Band

Ilikuwa raha kama kawa Mzalendo Pub ambapo Machozi Band huwa na maonesho kila Ijumaa, mwanamuziki muimbaji mahiri Lady JD akiwa na kundi lake zima la Machozi Band waliweza kuwapeleka wapenzi wa muziki katika safari ya kimuziki ya kona mbalimbali duniani, muziki toka Afrika , Ulaya, Amerika na raha pia kwa wapenzi wa muziki wa Reggae, mduara, rhumba, soukus alimradi kila mtu alipata dozi yake. Kila Alhamisi kundi zima liko NYUMBANI LOUNGE. Kukosa ni kosa
BJ band

King Maluu alikuwa katembelea BJ Band pia


Michael LilokoJuma Kakere
BJ Band huporomosha muziki kila Ijumaa pale Bussiness maeneo ya Victoria. Kundi zima chini ya uongozi wa Juma Kakere huleta muziki mchanganyiko ukisindikizwa na nyimbo zilizoutunzi wa Juma Kakere mwenyewe.

VIJANA WA TANZANIA HUENDA WAPI KUPUMZISHA AKILI BAADA YA SAA ZA KAZI?

AWALI HAPA PALIKUWA NA JENGO LILILOITWA  NYUMBA YA SANAA WASANII WENGI WALIKUWA WAKIFANYA KAZI ZAO HAPA, KWA SASA KILICHOBAKI JINA WASANII...