Saturday, October 15, 2011

Huu sasa ni uvivu wa kupindukia, na utovu wa nidhamu

Utajisikiaje pale ambapo umelipia pesa kumwona na kumsikiliza msanii unaempenda, na akisha panda jukwaani baada ya nyimbo 3 haonekani tena? Hadithi hiyo imeanza kulalamikiwa na wapenzi wa muziki  wa nchi kadhaa baada ya wasanii wetu kwenda huko na kufanya show zenye nyimbo 3 au 4 na kudai wamemaliza show na kuwaachia waandaji mtiti mzito kuhusu hali hiyo.  Kuna baadhi ya wasanii wetu maarufu wamepoteza heshima katika nchi kadhaa kutokana na kutokidhi hamu ya wapenzi wa muziki kwa kupiga chini ya nyimbo 5 katika show. Kulia ni orodha ya nyimbo 20 alizopiga Snoop Dogg kwenye show aliyopiga jana huko Oslo Norway. Ikiwa huyu msanii maarufu anafikisha hadi nyimbo 20 kwanini wasanii wetu wasizidi hapo?

Haji Ramadhani awa mshindi wa kwanza BSS 2011


Haji Ramadhani

Rogers Lucas
Waziri Salum
 Katika fainali zilizofanyika usiku wa kuamkia leo pale Diamond Jubilee jijini Dar, Haji Ramadhani amekuwa mshindi wwa kwanza na amefanikiwa kunyakua kitita cha shilingi mil 40 baada ya kutwaa taji la Bongo Star Search 2011.Mshindi wa pili akiwa Rogers Lucas na Waziri Salum akichukua nafasi ya tatu. Blog hii inawapa hongera wooote

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...