Huu sasa ni uvivu wa kupindukia, na utovu wa nidhamu

Utajisikiaje pale ambapo umelipia pesa kumwona na kumsikiliza msanii unaempenda, na akisha panda jukwaani baada ya nyimbo 3 haonekani tena? Hadithi hiyo imeanza kulalamikiwa na wapenzi wa muziki  wa nchi kadhaa baada ya wasanii wetu kwenda huko na kufanya show zenye nyimbo 3 au 4 na kudai wamemaliza show na kuwaachia waandaji mtiti mzito kuhusu hali hiyo.  Kuna baadhi ya wasanii wetu maarufu wamepoteza heshima katika nchi kadhaa kutokana na kutokidhi hamu ya wapenzi wa muziki kwa kupiga chini ya nyimbo 5 katika show. Kulia ni orodha ya nyimbo 20 alizopiga Snoop Dogg kwenye show aliyopiga jana huko Oslo Norway. Ikiwa huyu msanii maarufu anafikisha hadi nyimbo 20 kwanini wasanii wetu wasizidi hapo?

Comments