Thursday, April 21, 2011

JD awasili Norway tayari kwa show kali za kipindi cha Pasaka nchi mbalimbali Ulaya

Lady Jay Dee, atakuwa nchi mbalimbali Ulaya kufanya maonyesho ya muziki. Mwimbaji huyu ambaye pia ni mtunzi mzuri sana atakuwa na ratiba ifuatayo, atakuwa Norway na kufanya maonyesho Bergen April 21 na Oslo April 22. Kisha atakuwa Netherlands April 23, wakati April 24 atakuwa Ugiriki, na kurudi kaskazini tena hadi Sweden atakakofanya onyesho April 29...mlioko huko kukosa ni kosa

Msondo katika ziara ndeeefuuu

Mnyupe & Roma
Msondo ngoma Group 'Baba ya muziki' imepanga kufanya ziara ndefu katika mikoa mbalimbali kuanzia April 21 mwaka huu. Ziara hiyo itaanzia katika mji wa Morogoro ambapo bendi itatumbuiza Savoy Inn tarehe April 21 usiku na tarehe April 22 bendi itakua Iringa katika ukumbi wa New Life Night Club na tarehe 23 April bendi itakuwa Makambako katika ukumbi wa Midtown.
 Bendi itaelekea Songea mkoani Ruvuma ambako tarehe 24 April kutafanyika onesho kubwa katika ukumbi wa Serengeti Bar. Tarehe 25 pia kutakuwa na onyesho jingine hapohapo Songea. Tarehe 26 bendi itakuwa Tunduru, na tarehe 27 moto utawaka Masasi katika ukumbi wa MADEKO
Msondo watakuwa Newala April 29 katika ukumbi wa Blantaya, wakati kesho yake April 30 Msondo wataweka mambo hadharani katika ukumbi wa Oceanic wa mjini Lindi na kuanza kurejea Jijini Dar es Salaam.


Roma &Nzawisa


Wasiliana na Bendi mbalimbali

 1. Kilimanjaro Band- 0713 787878 na 0713 274747
 2. InAfrica Band- 0713 605495.
 3. Tanzanite-0713 447442 
 4. African Stars Band-0713377779 na 0713 606564
 5. Babloom -0713 535534
 6. TOT Band-0655981423
 7. B Band-0713 470072
 8. African Beat Band-0654 925588
 9. Bantu Group 0719 880333
 10. Jhiko Manyika-0713 367401
 11. Shada Group-0713 444422
 12. Msondo Group 0655 921223
 13. Wazee Sugu- 0713 311673
 14. Tanzania Band-0715 511424
 15. Mlimani Park- 0715 302771 


Yakwetu Band wanaendelea na mazoezi makali

Mazoezi makali yanaendelea katika ukumbi wa Makumbusho ambapo Yakwetu Band wanatunga na kufanya mazoezi vibao vyao. Ili kupata uzoefu wamemwalika mpiga sax wa miaka mingi alioko Mlimani Park kwa miaka mingi Yusuph Bernard awasindikize katika tungo zao. Na wamewaalika wanamuziki wa Kilimanjaro Band waje wasikilize nyimbo zao na kutoa ushauri kuhusu tungo hizo.