Yakwetu Band wanaendelea na mazoezi makali

Mazoezi makali yanaendelea katika ukumbi wa Makumbusho ambapo Yakwetu Band wanatunga na kufanya mazoezi vibao vyao. Ili kupata uzoefu wamemwalika mpiga sax wa miaka mingi alioko Mlimani Park kwa miaka mingi Yusuph Bernard awasindikize katika tungo zao. Na wamewaalika wanamuziki wa Kilimanjaro Band waje wasikilize nyimbo zao na kutoa ushauri kuhusu tungo hizo.







Comments