Skip to main content

Posts

Showing posts from January 28, 2013

Lady In Red upgraded matayarisho in full swing

Lady in Red 2013 itakuwa ni ya 9 toka fashion show hiyo ilipoanza. Mwaka huu show imeamua kupanda daraja kwa kuhusisha wabunifu wengi zaidi na kuboresha show hiyo. Ili kuwezesha hilo matayarisho yamekwisha anaza na Jumapili waandaaji, designers na models walikutana katika kiota cha maraha Nyumbani Lounge na kuwa na mazunguzo mbalimbali kuhusu matayarisho ya siku hiyo. Shughuli itakuwa SERENA HOTEL, Jumamosi,9 February 2013 kuanzia saa 2:00 Usiku , kiingilio kikiwa 20,000/- kwa mtu mmoja na 50,000/- kwa mtu mmoja VIP. LULU APEWA DHAMANA ...LAKINI.....

Msanii Elizabeth Michael'Lulu" anayekabiliwa na shtaka la kumuuwa msanii mwenzie Steven Kanumba, hatimae leo ameweza kupata dhamana itakayomuwezesha kuwa nje ya rumande wakati kesi yake ikiendelea. Pamoja na kuweza kupata wadhamini, Lulu amelazimika kuendelea kuwa rumande kwa siku nyingine kutokana na kutokukamilika kwa taratibu za kimahakama, ikitegemewa kuwa taratibu hizo zitakamilika kesho na kumuwezesha kuwa nje ya rumande. Lulu aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya dhamana, kupitia kwa  mawakili wake,  Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).Masharti ya dhamana aliyopewa ni kama ni kama ifuatavyo, sharti la kwanza ni wadhamini wawili ambapo kila mmoja, udhamini wake ni shilingi Milioni 20 za kitanzania, sharti la pili ni kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani, la tatu ni kutosafiri nje ya Dar es Salaam, kwa kipindi chote cha kesi, la nne ni kuhakikisha kwamba anafika mahakamani kila ta…