LULU APEWA DHAMANA ...LAKINI.....

Msanii Elizabeth Michael'Lulu" anayekabiliwa na shtaka la kumuuwa msanii mwenzie Steven Kanumba, hatimae leo ameweza kupata dhamana itakayomuwezesha kuwa nje ya rumande wakati kesi yake ikiendelea. Pamoja na kuweza kupata wadhamini, Lulu amelazimika kuendelea kuwa rumande kwa siku nyingine kutokana na kutokukamilika kwa taratibu za kimahakama, ikitegemewa kuwa taratibu hizo zitakamilika kesho na kumuwezesha kuwa nje ya rumande. Lulu aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya dhamana, kupitia kwa  mawakili wake,  Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).Masharti ya dhamana aliyopewa ni kama ni kama ifuatavyo, sharti la kwanza ni wadhamini wawili ambapo kila mmoja, udhamini wake ni shilingi Milioni 20 za kitanzania, sharti la pili ni kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani, la tatu ni kutosafiri nje ya Dar es Salaam, kwa kipindi chote cha kesi, la nne ni kuhakikisha kwamba anafika mahakamani kila tarehe ya mwanzo wa mwezi lakini pia kuhakikisha kwamba anapofika mahakamani awe na hao wadhamini wake.

Comments