Skip to main content

Posts

Showing posts from April 14, 2013

HADHARANI MSANII MAARUFU ANATEGEMEA USHIRIKINA

Ushikina ni moja ya mila za kawaida sana kwetu Tanzania. lakini mara nyingi huwa kuna dhana kuwa jambo hili washiriki wake ni watu wazima wa zamani na vijana wa kileo hawashiriki kabisa mambo haya.
Lakini taarifa zilizoifikia blog hii zinaonyesha kuwa jambo hili bado ni muhimu katika maisha ya vijana ambao kwa kila taswira wana maisha ambayo ni mfano kwa vijana wengine na wana majina yanayoheshimika katika jamii.
Taarifa zimefika za msanii maarufu kukesha usiku akifanya shughuli za uganga kwa mganga mmoja Mburahati, mganga huyo ambaye taarifa zinasema kuwa awali alizawadiwa pikipiki kwa kazi hiyo na karibuni kapewa gari aina ya Opa kama malipo kwa shughuli zake hizo. msanii huyo kabla alikuwa akifika hapo hata mchana lakini kutokana na kufahamika na kuona anasindikizwa na watoto wa mtaa mzima wakati akielekea kwa mganga akalazimu kubadili ratiba na kuanza kufika maeneo hayo baada ya giza kuingia
Habari za ziada ni kuwa wasanii wengi wenye heshima katika jamii huonekana kwa mganga huyo …

Ya mwaka.......Profesa Jay na Profesa Issa Shivji wakiwa pamoja jukwaani

Ilikuwa ni jioni ya furaha baada ya kumalizika kwa shughuli za Kigoda cha Mwalimu Nyerere, washiriki wakiwa na wageni wao kutoka nchi mbalimbali duniani walipokusanyika katika car Park iliyo jirani na kituo cha polisi cha Chuo Kikuu na kuwa na tafrija ambayo ilisindikizwa na muziki kutoka kilimanjaro Band. Na ndipo alipopanda jukwaani Profesa maarufu Tanzania, Profesa Issa Shivji, na alipokuwa jukwaani akamuona Profesa jay, hapo ndio akatanganza kuwa ' Nimemuona Profesa mwenzangu Profesa jay naomba apande jukwaani aseme neno'. Wa mitulinga hakufanya kosa alilianzisha akisindikizwa na bendi ya Kilimanjaro iliyompa beat, akaanza kuteremesha mistari, palikucha