Sunday, April 14, 2013

Ya mwaka.......Profesa Jay na Profesa Issa Shivji wakiwa pamoja jukwaani

Ilikuwa ni jioni ya furaha baada ya kumalizika kwa shughuli za Kigoda cha Mwalimu Nyerere, washiriki wakiwa na wageni wao kutoka nchi mbalimbali duniani walipokusanyika katika car Park iliyo jirani na kituo cha polisi cha Chuo Kikuu na kuwa na tafrija ambayo ilisindikizwa na muziki kutoka kilimanjaro Band. Na ndipo alipopanda jukwaani Profesa maarufu Tanzania, Profesa Issa Shivji, na alipokuwa jukwaani akamuona Profesa jay, hapo ndio akatanganza kuwa ' Nimemuona Profesa mwenzangu Profesa jay naomba apande jukwaani aseme neno'. Wa mitulinga hakufanya kosa alilianzisha akisindikizwa na bendi ya Kilimanjaro iliyompa beat, akaanza kuteremesha mistari, palikuchaWaziri Ally Profesa jay, Profesa Shivji, Babu Njenje, Shaaba MatrebleNo comments:

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...