Skip to main content

Posts

Showing posts from May 17, 2011

FFU wa Ngoma Africa Band jukwaani tena

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU yenye masikani yake nchini Ujerumani, inatazamiwa kutumbuiza katika maonesho ya Afrika & Orient  Festival, katika Burg Satzvey jirani na miji ya Bonn na Koln,nchini Ujerumani. Onyesho hilo litakuwa siku ya Jumamosi 28 Mei 201, kuanzia saa 1.00 usiku. Kamanda wa kikosi kazi hiko Ras Makunja wa FFU atakiongoza kuhakikisha kuwa gwaride la muziki linamfikia kila mshabiki. Bendi hiyo ina  wanamuziki wenye vipaji wakiwemo wacharaza magitaa wakali kama vile Chris-B, Said Jazbo Vuai, Maxime Buanda, na wengineo.
Wasikilize zaidi ukiingia www.reverbnation.com/ngomaafricaband au www.myspace.com/thengomaafrica
jiunge nao www.ngoma-africa.com
wasiliana nao kupitia contact@ngoma-africa.com