Friday, June 3, 2016

JOHN KITIME NDIE KATIBU MKUU MPYA WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA

-->

John Kitime Katibu Mkuu Shirikisho la Muziki Tanzania
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania leo amemtangaza John Kitime kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo. Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo ulifanyika mwezi wa pili na vyam 8 vya Shirikisho hilo kuchagua viongozi wake. Nafasi ya Katibu Mkuu ilikuwa wazi. John Kitime ni mwanamuziki wa bendi ya Kilimanjaro (Wananjenje), ambaye miaka ya 90 alikuwa Mwenyekiti wa CHAMUDATA na wakati huo chama kilikuwa katika ufanisi mkubwa wa kuweza hata kuwa na ushirikiano na mashirika ya miasaada ya nje yaliyowezesha chama hicho kupata misaada mbalimbali, na hata kufanya matamasha makubwa ya muziki. Pia Kitime ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki chama ambacho pia kimewezesha wanacham wake kupata bima ya Afya. Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Katibu Mkuu huyo alisema  kati ya mambo atakayoanza nayo ni kuimarisha Shirikisho kwa kuimarisha vyama wanachama wa Shirikisho, ikiwemo kuhamasisha kuanzishwa vyama vingine. Kuonyesha kuwa anania ya kutekeleza hizo mwisho wa mkutano huo aliwahamasisha waandishi wa habari za muziki kuanzisha chama chao. Vyama vilivyo wanachama wa Shirikisho la Muziki Tanzania ni Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania CHAMUDATA, Chama cha Muziki wa Rumba CHAMURUMBA, Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania CHAMUITA, Tanzania Folk Music Development Association TAFOMUDEA, Tanzania taarab Association TTA, Tanzania Urban Music Association TUMA   

MUSICIANS BOOTCAMP YAFANA SANA


Mwanzoni mwa mwezi  Mei Culture and  Development East Africa (CDEA) ilitoa tangazo la kualika wanamuziki katika kambi ya mafunzo waliiita  Musicians Boot Camp. Kambi hii iliwekwa katika hoteli ya kitalii ya Red Monkey iliyoko Jambiani Zanzibar. Wanamuziki 20 walichaguliwa kuhudhuria kambi hii wakiwa ni mchanganyiko wa wanamuziki waimbaji wapigaji wa ala za kisasa na kiasili na wasanii wa Hiphop. Katika kambi hiyo baadhi ya masomo waliyojifunza ni
Digital Strategy, ambapo wasanii walijifunza namna ya kuboresha ‘brands’ zao katika ulimwengu wa kifijitali. Darasa hili liliongozwa na Jude Clark, mwanzilishi wa Joose Digital. Pia kulikuweko na darasa dogo la matumizi yenye tija ya mitandao ya kijamii.  Yusuf Mahmoud, Mtendaji Mkuu wa Sauti za Busara aliongelea umuhimu wa kushiriki matamasha kwa wanamuziki wa Tanzania. John Kitime akatoa somo kuhusu Copyright, Copyleft na Creative Commons. Somo hili lilifuatiwa na somo kutoka kwa Bi Rebecca Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space, yeye aliongelea somo lililoitwa Digitization of heritage music. Kuingiza katika dijitali muziki wetu wa Urithi. Somo ambalo lilifuatiwa na somo kutoka kwa Profesa Mitchel Strumpf, Mkurugenzi wa Masomo wa Dhow Countries Music Academy, Zanzibar alipoongelea namna ya kutunza urithi wa muziki. Hatimae masomo yaliongezwa thamani na elimu kutoka kwa  Sam Jones wa(Soundthread), John Kagaruki wa (Eyecuemedia) and Philemon Noirret wa (crazy only/tropical sound studio Zanzibar, ambao walielezea mambo mbalimbali kuhusu kurekodi na kufanya maonyesho live na maadili yake. Hakika elimu hii ni muhimu kuwafikia wanamuziki wengi zaidi.
Picha za Jam Session baada ya masomo
 


 

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...