Mwanzoni mwa
mwezi Mei Culture and Development East Africa (CDEA)
ilitoa tangazo la kualika wanamuziki katika kambi ya mafunzo waliiita Musicians Boot Camp. Kambi hii iliwekwa
katika hoteli ya kitalii ya Red Monkey iliyoko Jambiani Zanzibar. Wanamuziki 20
walichaguliwa kuhudhuria kambi hii wakiwa ni mchanganyiko wa wanamuziki
waimbaji wapigaji wa ala za kisasa na kiasili na wasanii wa Hiphop. Katika
kambi hiyo baadhi ya masomo waliyojifunza ni
Digital Strategy, ambapo
wasanii walijifunza namna ya kuboresha ‘brands’ zao katika ulimwengu wa
kifijitali. Darasa hili liliongozwa na Jude Clark, mwanzilishi wa Joose Digital.
Pia kulikuweko na darasa dogo la matumizi yenye tija ya mitandao ya kijamii. Yusuf
Mahmoud, Mtendaji Mkuu wa Sauti za Busara aliongelea umuhimu wa kushiriki
matamasha kwa wanamuziki wa Tanzania. John Kitime akatoa somo kuhusu Copyright,
Copyleft na Creative Commons. Somo hili lilifuatiwa na somo kutoka kwa Bi
Rebecca Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space, yeye aliongelea somo lililoitwa Digitization
of heritage music. Kuingiza katika dijitali muziki wetu wa Urithi. Somo ambalo
lilifuatiwa na somo kutoka kwa Profesa Mitchel Strumpf, Mkurugenzi wa Masomo wa
Dhow Countries Music Academy, Zanzibar alipoongelea namna ya kutunza urithi wa
muziki. Hatimae masomo yaliongezwa
thamani na elimu kutoka kwa Sam Jones wa(Soundthread),
John Kagaruki wa (Eyecuemedia) and Philemon Noirret wa (crazy only/tropical
sound studio Zanzibar, ambao walielezea mambo mbalimbali kuhusu kurekodi na
kufanya maonyesho live na maadili yake. Hakika elimu hii ni muhimu kuwafikia wanamuziki
wengi zaidi.
Picha za Jam Session baada ya masomo
Comments