Thursday, February 23, 2012

Wahapahapa Jukwaaani Nafasi Art space

Wahapahapa Band
Wahapahapa Band wameweka lengo la kupiga kila mwisho wa mwezi Nafasi Art space.Bendi hii ambayo hupiga muziki mseto wa kiasili ya Tanzania,ina mkusanyiko wa kati ya wanamuziki mahiri katika nchi hii. Ni wazi kuhudhuria maonyesho haya ni ufunguo mkubwa wa kupata vionjo vya Utanzania.

Ijue Inafrika Band

Roy Figueiredo
Bizimana Ntavyo
The Inafrika band ilianzishwa mwaka 1992 na ndugu wawili Enrico and Roy Figueiredo . Bendi ilianza has akama bendi iliyokuwa ikipiga muziki wa kunakili toka kwa bendi nyingine(Cover band). Kwa hiyo kwa muda mrefu ilipiga katika mahoteli na migahawa mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam kama vile Cassanova, Smokies Tavern, Arcade, Wet ‘n’ Wild na kadhalika, kwa muda mrefu bendi ilikuwa ikifanya maonyesho katika kumbi za hotel kubwa ya Kilimanjaro Hotel.

Nurdin Athuman
Katika mwaka wa 1996 bendi iliweza kufanya maonyesho katika sehemu mbalimbali na wasanii wa kimataifa kama YVONNE CHAKA CHAKA,MWALE SISTERS, SARAFINA.
Hamis Mlenge
Ritchie Mwanisawa
Pompidou Dominic
Mwaka 2000 bendi ilipata msukosuko kiasi cha kuvunjika na kuanza upya na hapo mwaka 2001 ikarekodi album yake ya kwanza iliyotambulika kwa jina la Indege, nyimbo ya Indege iliweza kupata tuzo la Kilimanjaro Music Award mwaka 2003/4 katika kundi la nyimbo bora ya kiasili (Best Traditional Song). Bendi ilikuwa na umaarufu kiasi cha kuweza kusindikiza Mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka kadhaa. Na kutumbuiza katika mikusanyiko kadhaa ikiwemo mkusanyiko wa Wabunge wa Tanzania. Bendi ilizunguka nchi mbalimbali ikiwemo South Korea, Afrika ya Kusini, United Arab Emirates, visiwa vya Comoro na Mayotte. Kwa sasa bendi iko katika maonyesho yanayozunguka nchi mbalimbali duniani yanajulikana kama MOTHER AFRICA SHOW yenye makao makuu Hamburg, Ujerumani. Bendi imekuwa katika hii show kwa kuanzia mwaka 2006 na imeshafanya maonyesho Ulaya , Australia na Asia. Na kwasasa imetoa album mpya kabisa inaitwa Mbeleko. Wanmuziki wa Inafrika ni wafuatao:-

1. Bizimana Ntavyo - keyboards,vocals
2. Roy Figueiredo -Band leader,Bass,vocals.
3. Nurdin Athumani - lead guitar,vocals.
4. Pompidou Dominic- percussion,vocals.
5. Ritchie Mwanisawa-drums vocals
6. Hamisi Mlenge - Saxaphone,trumpets, flute,vocals.
7. Steve John - Lead vocals.


Mashujaa Band Club SunCiro

Haya wapenzi wa Mashujaa Band, kila Alhamisi watakuwa Club Sun- Ciro Msikose masebene ya nguvu.

Leah muddy na Q Band wakiwa mazoezini

The Q Band wakiwa katika mazoezi makali kuendeleza bendi yao inayoongozwa na Leah Muddy yule binti aliyemaliza mashindano ya BSS akiwa na mimba kubwa lakini kushangaza watu kwa kuimbaa vizuri sana. Bendi hii kwa kawaida kila Alhamisi wako Maryland Bar Mwenge na Jumamosi Sunset Beach Kigamboni.


Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...