![]() |
| Roy Figueiredo |
![]() |
| Bizimana Ntavyo |
![]() |
| Nurdin Athuman |
![]() |
| Hamis Mlenge |
![]() |
| Ritchie Mwanisawa |
![]() |
| Pompidou Dominic |
Mwaka 2000 bendi ilipata msukosuko kiasi cha kuvunjika na kuanza upya na hapo mwaka 2001 ikarekodi album yake ya kwanza iliyotambulika kwa jina la Indege, nyimbo ya Indege iliweza kupata tuzo la Kilimanjaro Music Award mwaka 2003/4 katika kundi la nyimbo bora ya kiasili (Best Traditional Song). Bendi ilikuwa na umaarufu kiasi cha kuweza kusindikiza Mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka kadhaa. Na kutumbuiza katika mikusanyiko kadhaa ikiwemo mkusanyiko wa Wabunge wa Tanzania. Bendi ilizunguka nchi mbalimbali ikiwemo South Korea, Afrika ya Kusini, United Arab Emirates, visiwa vya Comoro na Mayotte. Kwa sasa bendi iko katika maonyesho yanayozunguka nchi mbalimbali duniani yanajulikana kama MOTHER AFRICA SHOW yenye makao makuu Hamburg, Ujerumani. Bendi imekuwa katika hii show kwa kuanzia mwaka 2006 na imeshafanya maonyesho Ulaya , Australia na Asia. Na kwasasa imetoa album mpya kabisa inaitwa Mbeleko. Wanmuziki wa Inafrika ni wafuatao:-1. Bizimana Ntavyo - keyboards,vocals
2. Roy Figueiredo -Band leader,Bass,vocals.
3. Nurdin Athumani - lead guitar,vocals.
4. Pompidou Dominic- percussion,vocals.
5. Ritchie Mwanisawa-drums vocals
6. Hamisi Mlenge - Saxaphone,trumpets, flute,vocals.
7. Steve John - Lead vocals.






Comments