Wednesday, January 23, 2013

MSONDO NGOMA YAFIWA NA MPIGA BEZI

Bendi ya Msondo Ngoma Music Band jioni hii imempoteza mpiga gitaa la bezz Ismail Mapanga, Hali yake ilianza kudhoofu wakati bendi ikiwa katika safari mkoani Tabora wiki iliyopita.
Taratibu za mazishi zitakapotolewa tutatoa taarifa
 
                           MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI

WASANII WAIJIA JUU COSOTA NA BODI YA FILAMU

SHESHE la aina yake limeibuka baada ya wasanii wa filamu nchini kutoa tamko kuwataka viongozi wa Chama cha Hakimiliki (COSOTA) na Bodi ya filamu kuachia ngazi kutokana na kushindwa kushughulikia matatizo yao......Hayo ndio maelezo kutoka katika gazeti moja la kila wiki kuhusu mvutano kati ya wasanii wa filamu na viongozi hawa wawili. Katika vipindi viwili vya TV vilivyorushwa TBC na kingine EATV, ambacho kilikuwa 'live', wasanii chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji nchini Mike Sangu, waliueleza ulimwengu juu ya adha wanazozipata kutokana na vipengele vilivyomo katika Kanuni za Bodi ya filamu, na pia kueleza jinsi wasivyo na imani na Justus Mkinga, Mtendaji Mkuu wa COSOTA. Kwa maelezo a picha zaidi ingia HAPA

IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...