Thursday, May 16, 2013

COSOTA YAKUTANA NA WASANII

Wasanii kadhaa wakiwemo viongozi wa Mashirikisho ya Muziki na Filamu, wasanii binafsi, wawakilishi wa wasanii, viongozi wa vyama vinavyohusika na sanaa, jana Alhamisi tarehe 16 May walikusanyika pamoja katika ofisi za COSOTA na kuwa na mazungumzo yenye kujaribu kujenga ukaribu wao , na kutafuta njia za kulinda na kufaidika na kazi za wasanii wa Tanzania. Kati ya mambo yaliyozungumzwa ni mikakati ya COSOTA katika kupambana na Uharamia wa kazi za sanaa, kuboresha ukusanyaji wa mirabaha, ikiwemo na kutafuta njia ya kulazimisha vyombo vya utangazaji kulipia mirabaha kwa kazi za muziki, na pia kuangalia sura ya mbele ya ulinzi wa Hakimiliki. Tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali mazungumzo yalikuwa yaki utu uzima yaliyofikia mwafaka wa kuendeleza mazungumzo ya aina hii. COSOTA waliombwa kutengeneza mazingira ya kuwa na mkutano mkubwa wa wananchama wote, hasa ikizingatiwa kuwa mkutano wa mwisho ulikuwa 2007.


Mwakifamba Rais wa Shirikisho la Muziki

Muyamba, Mwenyekiti wa Wasambazaji

Inno Nganyagwa Mwanamuziki

Muumin Mwinyjuma Mwanamuziki


Stela Mwanamuziki wa Muziki wa Enjili

MASHINDANO YA KIGOLI WA TZ 2013 YATANGAZWA RASMI...KITIME MMOJA WA MAJAJI


Mashindano ya Kigoli wa TZ 2013 yaliyotayarishwa na mtangazaji maarufu Maimatha wa Jesse yametangazwa rasmi katika ukumbi wa The Olympia, paleeee Sinza Mori. Waandishi mbalimbali  walipata taarifa juu ya shindano hili litakalojumuisha mabinti wa kuanzia umri wa miaka 18 hadi 28, ambalo litazinduliwa rasmi tarehe 31 May, 2013 na kufikia kilele mwanzoni mwa mwezi July.
Majaji wa mashindano hayo ambayo pia yatashirikisha mabinti kutoka Morogoro na Tanga watakuwa Maimatha, John Kitime, na Musa wa Kitaa