Wasanii kadhaa wakiwemo viongozi wa Mashirikisho ya Muziki na Filamu, wasanii binafsi, wawakilishi wa wasanii, viongozi wa vyama vinavyohusika na sanaa, jana Alhamisi tarehe 16 May walikusanyika pamoja katika ofisi za COSOTA na kuwa na mazungumzo yenye kujaribu kujenga ukaribu wao , na kutafuta njia za kulinda na kufaidika na kazi za wasanii wa Tanzania. Kati ya mambo yaliyozungumzwa ni mikakati ya COSOTA katika kupambana na Uharamia wa kazi za sanaa, kuboresha ukusanyaji wa mirabaha, ikiwemo na kutafuta njia ya kulazimisha vyombo vya utangazaji kulipia mirabaha kwa kazi za muziki, na pia kuangalia sura ya mbele ya ulinzi wa Hakimiliki. Tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali mazungumzo yalikuwa yaki utu uzima yaliyofikia mwafaka wa kuendeleza mazungumzo ya aina hii. COSOTA waliombwa kutengeneza mazingira ya kuwa na mkutano mkubwa wa wananchama wote, hasa ikizingatiwa kuwa mkutano wa mwisho ulikuwa 2007.
Mwakifamba Rais wa Shirikisho la Muziki |
Muyamba, Mwenyekiti wa Wasambazaji |
Inno Nganyagwa Mwanamuziki |
Muumin Mwinyjuma Mwanamuziki |
Stela Mwanamuziki wa Muziki wa Enjili |
Comments