Skip to main content

Posts

Showing posts from October 27, 2011

Twanga Festival 2011 kuwa Jumapili 6 November, Leaders Club

Wasanii mbalimbali wa fani ya muziki wenye majina hapa Nchini, wamethibitisha kushiriki katika Tamasha la Twanga Pepeta (Twanga Festival 2011) litakalofanyika siku ya Jumapili ya tarehe 06-11-2011 katika viwanja vya Leaders vilivyopo maeneo ya Kinondoni. wasanii hao ni pamoja na Isha Mashauzi akiwa na kundi lake la Mashauzi Classic, Msondo Ngoma Music Band, Schengen Academy na Prince Dully Sykes. aidha kuna wasanii wengi ambao bado ASET ipo katika mazungumzo nao ili wafanye shoo katika Tamasha hilo.
Tamasha hilo ambalo sehemu kubwa litahusisha uzinduzi wa albamu ya 11 ya  Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" inayojulikana kwa jina la "Dunia Daraja". Albamu itakuwa na nyimbo sita ambazo ni "Dunia Daraja" yenyewe iliyotungwa na Charlz Baba, "Penzi la Shemeji" imetungwa na Prince Mwnjuma Muumini, "Mtoto wa Mwisho" imetungwa na Dogo Rama, Kiongozi wa Bendi Bi Luizer Mbutu yeye ametungw a wimbo "Umenivika Umasikini", Kiongozi Msaid…