Wasanii mbalimbali wa fani ya muziki wenye majina hapa Nchini, wamethibitisha kushiriki katika Tamasha la Twanga Pepeta (Twanga Festival 2011) litakalofanyika siku ya Jumapili ya tarehe 06-11-2011 katika viwanja vya Leaders vilivyopo maeneo ya Kinondoni. wasanii hao ni pamoja na Isha Mashauzi akiwa na kundi lake la Mashauzi Classic, Msondo Ngoma Music Band, Schengen Academy na Prince Dully Sykes.
aidha kuna wasanii wengi ambao bado ASET ipo katika mazungumzo nao ili wafanye shoo katika Tamasha hilo.
Tamasha hilo ambalo sehemu kubwa litahusisha uzinduzi wa albamu ya 11 ya Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" inayojulikana kwa jina la "Dunia Daraja". Albamu itakuwa na nyimbo sita ambazo ni "Dunia Daraja" yenyewe iliyotungwa na Charlz Baba, "Penzi la Shemeji" imetungwa na Prince Mwnjuma Muumini, "Mtoto wa Mwisho" imetungwa na Dogo Rama, Kiongozi wa Bendi Bi Luizer Mbutu yeye ametungw
a wimbo "Umenivika Umasikini", Kiongozi Msaidizi Saleh Kupaza yeye ametunga wimbo "Kiapo cha Mapenzi" na wimbo Kauli wa Rogart Hegga kabla ya kuhama.
wiki ijayo katika nia ya kujiandaa vilivyo na Tamasha ili kuwapa wapenzi wake burudani ya uhakika Twanga Pepeta inataraji kuingia kambini katika sehemu itakayotangazwa hapo baadae na kwa sasa wanafanya matayarisho ya awali katika mazoezi yanayoendelea katika ofisi za ASET zilizopo Kinondoni nyuma ya Ukumbi wa Mamngo Garden uliopo Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Albamu mpya imeongezewa nguvu na ujio wa wanamuziki wapya walioshiriki kikamilifu katika utengenezaji na hatimaye kurekodi nyimbo 4 ambazo ni Penzi la Shemeji, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na umenivika umasikini. wanamuziki hao wapya ni Mwinjuma Muumini aliyetokea Bwagamoyo Sound, Venance Joseph, pia katokea Bwagamoyo Sound, Grayson Semsekwa na Khadija Mnoga waliotokea Extra Bongo, mpiga gitaa la Solo Selemani Shaibu aliyetokea Akudo Impact na jumanne Said aliyetokeakwenye Bendi ya Ellystone Angai.
hii itakuwa ni mara ya tatu kwa twanga pepeta kufanya uzinduzi wake tofauti na Ukumbi wa Diamond uliokuwa ukizoeleka kwa kufanyia zinduzi za albamu zake, uzinduzi wa kwanza wa Kisa cha Mpemba uliofanyika mwaka 1999 ulifanyika katika ukumbi wa Mango Garden, halikadhalika na uzinduzi wa Jirani uliofanyika mwaka 2000 pia ulifanyika ukumbini hapo Mango Garden. Zinduzi zote zilizofuatia za Fainali Uzeeni mwaka 2001, Chuki Binafsi mwaka 2002, Ukubwa Jiwe mwaka 2003, Mtu Pesa mwaka 2004, Safari 2005 mwaka 2005, Password mwaka 2006, Mtaa wa kwanza mwaka 2007 na Mwana Dar es salaam mwaka 2009 zote hizo zilifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
HASSAN REHANI.
MRATIBU WA TAMASHA.
Comments