Friday, November 16, 2012

MONALISA ATOKELEZEA TENA


MASHUJAA MUZIKA NA JB MPYANA JUKWAA MOJA 30.11.2012

Katika kukamilisha uzinduzi wao wa album ya'Risasi Kidole', Mashujaa Band watakuwa na onyesho kubwa linalotegemewa kufanyika viwanja vya Leaders tarehe 30 November 2012. JB Miana na kundi lake watakuwa jukwaaa moja na bendi hii. Mambo matamu yanakuja.


MSONDO WAANZA KUTUMIA VYOMBO VIPYA

Maspika mapya


Msondo wameanza kutumia vyombo vipya, nimehudhuria onyesho lao kuna tofauti kubwa sana, ni wazi  utamu wa msondo umeongezeka sana sana. Aksante sana Konyagi kwa vyombo hivyo.

CHIKU KETO MDADA MWINGINE KATIKA HIP HOP TANZANIA

 Chiku Keto si jina geni sana katika anaga za muziki wa Bongofleva, alianza kujulikana zaidi hasa baada ya kuingia katika mpambano wa BSS na kutolewa kasha kurudishwa na baadae kukosa kura za kutosha na kutoka tena jambo ambalo mpaka leo mwenyewe anasema lilimuuma sana maana aliona kama kiini macho fulani. Chiku alizaliwa miaka kadhaa iliyopita katika hospitali ya Ocean Road tarehe 18 Aprili. Baba yake alikuwa Afisa Elimu kwa hiyo alikuwa katika maisha ya kuhama akifuatana na baba yake kila alipohamishwa. Hili lilisababishwa asome shule za msingi morogoro na Lindi. Alipata elimu ya sekondari katika shule ya Sekondari ya Mkonge huko Lindi, na baada ya hapo kurudi Dar es Salaam ambapo wazazi wake walirudi kuishi baada ya baba yake kustaafu. Baada ya kumaliza masomo ya sekondari alijiunga na chuo cha Uandishi cha Royal School of Journalism kilichopo Ubungo, baada ya kupata cheti, akajiunga na VETA na kufanya kozi ya ufundi wa magari kwa mwaka mmoja ambapo pia alipata Certificate ya utaalamu huo. Mzuka wa muziki ulikuwa taratibu umeshamuingia kwani 2005 aligonga hodi Baucha Records na kurekodi kibao kilichoitwa ‘Fungua Mlango’, ambacho pamoja na kukisambaza kwenye radio kadhaa, hakikupigwa kamwe. Mwaka 2006 akajitosa katika mashindano ya BSS, ambapo alifanya vyema na kuweza kuingia katika top ten ya washiriki, lakini akatolewa, na kwa mapendekezo ya ‘Chief Judge’ aliweza kurudi kwenye kinyang’anyiro lakini akatolewa tena kutokana na kutokuwa na kura za kutosha. Aliomba msaada wa uongozi wa Benchmark kwenda kurekodi wimbo ka thamani ya shilingi laki mbili katika studio za Double B, nyimbo hiyo pia haikuweza kutoka. Hatimae akajisogeza Dhahabu Records ya Dully Sykes ambapo aliweza kurekodi nyimbo kadhaa lakini hazikujulikana kutokana na kukosa mtu wa kuzisimamia katika promotion na kadhalika. Alihama hapo na kujiunga na kundi lililokuwa likiendeshwa na Chidi Benz. Aliweza kuzunguka sehemu nyingi za nchi na nje ya nchi kama supporting artist wa Chidi Benz, na katika kundi hili alilokaa miaka minne aliweza kushiriki nyimbo kadhaa zikiwemo ‘Muda umefika na Why. Aliliacha kundi hili na sasa yuko kundi la ARM Entertainment ambapo amekwisha rekodi wimbo wa Natafuta na Mzuka. Chiku amekwisha fanya kazi pia na mwanamuziki Lady Bee kutoka Kenya, mwanamuziki huyo kwa sasa amebadili muelekeo na anajihusisha na muziki wa Gospel…Chiku Keto bado yuko safarini

LADY JAY DEE KUJA NA KIPINDI KIPYA CHA KWENYE TV


Mwanamuziki  muimbaji mahiri Judith Wambura (kulia) maarufu kwa jina la Lady Jay Dee ametambulisha rasmi  kipindi chake kipya cha luninga kitakachoitwa ‘Diary ya Lady Jay Dee’.
Mkuu wa Vipindi wa East Africa TV Bi. Lydia Igarabuza(kushoto), akiwa na Lady Jay Dee
Jay Dee amesema madhumuni ya kipindi hicho ni kuleta burudani tofauti kwa wapenzi wa muziki wake, na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla, vilevile kitatoa fundisho na changamoto kwa wasanii chipukizi kujua wasanii wakongwe wamepitia katika vikwazo gani.
 Kipindi hicho kitakuwa hewani East africa Tv-Channel 5, Jumapili saa 3 usiku kuanzia Novemba 18.2012

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...