Monday, November 12, 2012

MUIMBAJI MARIAM KHAMIS WA TOT TAARAB AFARIKI DUNIA

-->

MWIMBAJI nyota wa taarab nchini, Mariam Khamis aliyekuwa katika kikundi cha TOT Taarab, amefariki dunia katika hospitali ya Muhimbili baada ya kujifungua usiku wa leo. Mariam alijiunga na TOT akitokea katika kundi la  Five Stars Modern Taarab.
Mariam, ambaye aliwahi kutamba kwa kibao chake cha ‘Paka mapepe’,  mbali na kuimbia kundi la Five Stars, Mariam pia aliwahi kung’ara alipokuwa katika vikundi vya East African Melody na Zanzibar Stars.Baadhi ya vibao alivyotamba navyo katika vikundi hivyo ni pamoja na ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.
Mungu ailaze pema roho ya Mariam

MTANGAZAJI LULU OSCAR AFARIKI DUNIA


Lulu Oscar binti mchangamfu ambaye kwa karibuni alikuwa mtangazaji wa SIBUKA TV akiendesha kipindi cha Pepeta Afrika, ambacho alikifanya mara nyingi akiwa na mwanamuziki Hamza Kalala, na ameweza kuwahoji wanamuziki wengi sana wa aina zote za muziki, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Lulu alikuwa anaumwa siku za karibuni, na alikuwa amelazwa hospitali.
Lulu alikuwa mchangamfu na mcheshi mwenye kupenda sana utani, nilimfahamu awali akiwa mtangazaji katika radio moja kule Njombe, ambapo hatimae aliamua kuhamia Dar es Salaam kutafuta maisha na akapata kazi Sibuka TV.
Mungu Amlaze peponi pema Amen