Skip to main content

Posts

Showing posts from March 26, 2013

VITUKO VYA VIONGOZI WA MABENDI 2

Mapenzi kazini mara nyingi ni tatizo, hasa pale maamuzi ya kikazi yanapoanza kuingiliwa namahusiano ya kimapenzi. Katika mabendi kadhaa tatizo hili limejitokeza na mara nyingine kuvunja bendi kabisa. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo kiongozi wa bendi ndie mmoja wa wahusika. Najua watu mawazo yao yanalenga kwa viongozi wanaume kuwa na mpenzi mfanyakazi mwanamke, kiukweli hali si lazima kila mara iwe hivyo kama ntakavyowaeleza baadae. Nianze na matukio yaliyonikuta miaka mingi iliyopita nikiwa katika bendi moja ambapo kiongozi wa bendi alijikuta katika mapenzi mazito na mcheza show katika bendi. Mheshimiwa huyu alikwisha kabisa kiasi cha kutumia muda wa mazoezi akiwa guest house na huyu binti hasa kwa kuwa alikuwa na mke nyumbani kwake. Kiongozi aliacha kabisa kufanya mazoezi na hata binti pia akawa akija kazini ni kama anakuja kwa kiongozi. Kuna siku tulikuwa na onyesho Morogoro, binti akagoma kuja, kiongozi alikuwa kama mgonjwa akamtuma mcheza show mwanaume ambembelezee binti a…