Wednesday, June 19, 2013

MAONYESHO YA LADYJD NA MWANAFA WANAMUZIKI WAMEJIFUNZA NINI?

Kuna somo ambalo liko wazi kabisa. Vikundi vyetu vingi hufanya hata zaidi ya maonyesho matano kwa wiki, na kupata mapato kiduchu, mara nyingine hata fedha ya usafiri kuwarudisha wanamuziki nyumbani baada ya onyesho haipatikani. Lakini tumeona kuwa maonyesho haya makubwa yaliyopangwa na kutayarishwa vizuri na pia kupewa promo ya kutosha huweza kuingiza kipato katika siku moja ambacho ni sawa na mapato ya miezi kadhaa ya vikundi vyetu katika mtindo wa sasa wa maonyesho ya kila siku yasiyo na matayarisho ya kutosha. Wanamuziki tutafakari!!!!!!!!!!!!!!

IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...