Wednesday, June 19, 2013

MAONYESHO YA LADYJD NA MWANAFA WANAMUZIKI WAMEJIFUNZA NINI?

Kuna somo ambalo liko wazi kabisa. Vikundi vyetu vingi hufanya hata zaidi ya maonyesho matano kwa wiki, na kupata mapato kiduchu, mara nyingine hata fedha ya usafiri kuwarudisha wanamuziki nyumbani baada ya onyesho haipatikani. Lakini tumeona kuwa maonyesho haya makubwa yaliyopangwa na kutayarishwa vizuri na pia kupewa promo ya kutosha huweza kuingiza kipato katika siku moja ambacho ni sawa na mapato ya miezi kadhaa ya vikundi vyetu katika mtindo wa sasa wa maonyesho ya kila siku yasiyo na matayarisho ya kutosha. Wanamuziki tutafakari!!!!!!!!!!!!!!

1 comment:

samson Mwasakafyuka said...

mimi somo nililoliona ni moja ni moja .
Onesho/onyesho la JD linapaswa kuwafumbua macho wasanii kuwa kulialia wanaonewa na jamaa wa mawingu ni ufala na ujinga, wanapaswa kutumia media zingine kutafuta Promo ambayo itawatoa,

Wakiwa wajinga hawataliona hili, wataendelea kuwanyenyekea mawingu na wasipofikia Lengo lao watakuja kulialia.
Mawingu ni Mapebari kama walivyo wengine Lengo lako ni capital maximization.

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...