Skip to main content

Posts

Showing posts from March 28, 2017

BASATA YATOA ZAWADI KWA WALIOFANYA VIZURI MASOMO YA SANAA KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

Kwamara ya kwanza Baraza la Sanaa la Taifa limetoa tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihano wa Taifa wa kidato cha nne. Utaratibu huu uliwahi kuweko miaka mingi iliyopita lakini tuzo zilienda tu kwa waliohitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka mingi iliyopita.Wanafunzi bora katika mitihani ya sanaa kutoka shule za sekondari za Makongo, Loyola, Azania zote za Dar es Salaam, Arusha Secondary, Bukoba Secondary na Darajani Secondary ya Kilimanjaro, walipata veti na kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi 250,000/- na pia Shirikisho la Sanaa za Ufundi liliongeza a vifaa vya kuchorea kwa washindi hao. Washindi hawa ndio waliokuwa wanafunzi bora katika mitihani yao Kitaifa. Shule ambazo wanafunzi hawa walitoka pia zilipata vyeti na waalimu wa masomo pia walipata tuzo. Washiriki walisimama kwa dakika moja kumkumbuka mwalimu wa sanaa Sister Elizabeth Justin ambaye alikuwa mwalimu wa muziki wa shule ya Loyola na ambaye kwa miaka miwili mfululizo alitoa wanafunzi bora K…