Skip to main content

Posts

Showing posts from October 3, 2011

Wasanii wa Tanzania na alama za Kishetani

Katika shughuli za sanaa ile ambayo ni ya mapokeo kwa mfano muziki , filamu na kadhalika, wasanii hujikuta wanaiga mambo mengi kutoka kwa wale ambao wanawachukulia kama ni mfano wa mafanikio. Wasanii wa hapa nchini hawapo tofauti na wasanii wenzao wa sehemu nyingine kwani nao pia huiga mengi kutoka kwa wasanii wanaoona hasa kutoka nchi za Magharibi. Uvaaji, ulaji unywaji, na maisha kwa ujumla. Lakini katika kuiga huko kuna mengi yanaigwa ambayo wasanii ingekuwa vyema kama wangefahamu maana yake kwani si nzuri hata kidogo. Katika historia ya wasanii kumekuwepo na hadithi nyingi za wasanii kuuza roho zao kwa shetani , au kuabudu shetani (Devil Worship), ili waweze kupata mafanikio kisanii. Uanachama wa Illuminati, Devil Worship, Satanism(Kanisa la shetani), 666 na kadhalika, umekuwa unatajwa kuhusiana na watu maarufu wengi kati nchi za magharibi. Ili kuonyesha uhusiano wao na vikundi hivi wasanii hawa huonyesha alama nyingi kwa kutumia miili yao au hata katika picha za album zao au manen…