Skip to main content

Posts

Showing posts from February 22, 2012

Mchango wa Radio katika utamaduni wa Tanzania

Mwaka 1951 afisa mmoja wa BBC alipendekeza kuanzishwakwa redio katika koloni la Uingereza la Tanganyika, ili kupata ujuzi wa kutengeneza vipindi kwa ajili ya wenyeji wanchi hii. Serikali ya Uingereza ikatoa kiasi cha dola 30000 na Dar es Salaam Broadcasting Station ikazaliwa. Redio ilianza na kutangaza kipindi kimoja cha Kiswahili kwa wiki, hii ikapanda kwa kipindi hicho kurudiwa mara mbili kwa wiki. Kutokana na uhafifu wa mitambo, ilikuwa vigumu kusikia matangazo hayo hata nje ya Dar es salaam tu. Taratibu vipindi vikaongezwa na mitambo ikaboreshwa na hatimae jina likabadilishwa na radio hiyo kuitwa Tanganyika Broadcasting Service. Kufikia 1954 pamoja na mapungufu mengi ya vifaa, radio ilikuwa na wataalamu wote wenyeji, lakini ilikuja kuwa na mafanikio ambayo yalikuwa kama kwa nchi nyingine nyingi zilizokuwa ni koloni za Uingereza. Mwaka 1961 bila kumwaga damu Tanganyika ikapata Uhuru chini ya uongozi wa Mwalimu J ulius Nyerere na chama chake cha TANU. Serikali mpya ikaona redio ni k…