Skip to main content

Posts

Showing posts from May 30, 2013

TANGAZO LA AIRTEL KUUZA NYIMBO ZA MANGWEA- JE NI MUDA MUAFAKA? AU NDIO KUFA KUFAANA?

JAY Z ALIPOAMUA KUUCHANA KI HIP HOP UONGO WA KIHISTORIA

Na Moses Gasana Mwezi wa nne mwaka huu wanamuziki Jay Z na Beyonce, ambao ni mume na mke wakibarikiwa kuwa na mtoto mmoja, walifanya safari ya kwenda Cuba kwa mapumziko katika kusherehekea miaka mitano ya ndoa yao. Safari hiyo iliibua mjadala mkubwa miongoni mwa raia wa Marekani na watu wengine wa Ulaya, Amerika ya Kusini, Asia na Afrika.


Kilicholeta mjadala miongoni mwa Wamarekani wenyewe kuhusu safari ya Jay Z na Beyonce ni kutokana na ukweli kuwa kuna masharti magumu ya kisheria ili mtu aweze kuruhusiwa kwenda nchini Cuba. Hii ni kutokana na kuwa kwa miaka 51 kisiwa cha Cuba kimekuwa chini ya vikwazo vya kiuchumi kutoka kwa serikali ya Marekani. Mojawapo ya vikwazo hivyo ni kwamba raia wa Marekani haruhusiwi kusafiri kwenda Cuba kama safari yake hiyo haihusiani na masuala ya elimu, utamaduni au misaada ya kibinadamu. Sasa kwa safari ya Jay Z na Beyonce swali ikawa ‘imekuwaje hawa wapenzi tunaona wako Cuba kama watalii, wakati safari ya utalii hairuhusiwi?’. Hapa lazima uzingatie kuwa…

P FUNK WA BONGO RECORDS AMUONGELEA MANGWEAR