Tuesday, November 20, 2012

LADY JAY DEE KATIKA MAZOEZI YA PIANO
Leo nimepata bahati ya kumkuta mwanamuziki mmoja nimpendae akifanya mazoezi kuongeza kipaji kingine juu ya vingi alivyonavyo. Nimemkuta Lady Jay Dee akiwa kwenye mazoezi makali ya kupiga piano. Msanii anaejitambua ndie huwa anafanya mazoezi, na ni mara chache sana msanii wa hapa kwetu aliyefikia ngazi aliyofikia Jay Dee kuhangaika kujifunza kitu kipya. Hongera mama kwa kutuonyesha njia.

IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...