Tuesday, February 14, 2012

Anania akipiga gitaa na kuimba wimbo wa Blue Suede Shoes

Anania ni mkalia , anaweza kupiga vyombo vingi vya muziki , vikiwemo gitaa, kinanda, kalimba na kadhalika. Hapa hebu tumsikilize akipiga wimbo wa zamani wa Rock n Roll Blue Suede Shoes ambao umekwisha rekodiwa na wanamuziki kama Elvis Presley, Cliff Richard na wengi wa Enzi hizo

Valentine Day nilipita Kalunde Band

Nilikaribishwa na rafiki yangu Anania Ngoliga kwenye bendi aliyopo wakati wakipiga katika siku ya Wapendanao. Binti mpya katika tasnia Bi Shilole alikuweko pia. Mambo yalikuwa mambo japo Kalunde ilikuwa imepoa si kama ile Kalunde ya miezi kadhaa iliyopita. Lazima kuweko na mabadiliko au lah safari haielekei kuzuri.

Anania Ngoliga

Mwanamuziki mualikwa Shilole


Bob Ludala

Deo Mwanambilimbi

Sarafina-Vocals

Waimbaji wa Kalunde, Mwapwani na Deborah

JUDITH KIULA MUIMBAJI MPYA WA GOSPEL

Judith Kiula ni mwenyeji wa Singida aliyezaliwa na kukulia Morogoro,  alizaliwa Kizuka hospital, na akaanza shule Kizuka primary school, ...