Nilikaribishwa na rafiki yangu Anania Ngoliga kwenye bendi aliyopo wakati wakipiga katika siku ya Wapendanao. Binti mpya katika tasnia Bi Shilole alikuweko pia. Mambo yalikuwa mambo japo Kalunde ilikuwa imepoa si kama ile Kalunde ya miezi kadhaa iliyopita. Lazima kuweko na mabadiliko au lah safari haielekei kuzuri.
Comments