Skip to main content

Posts

Showing posts from February 12, 2012

Mapacha Watatu....Mzalendo Pub

Huwa napata faraja sana kuwasikiliza Mapacha Watatu. Jumapili hii nilisindikizana na Mzee wa Madongo , Komando Hamza Kalala. Tukafika Mzalendo na haraka tukapanda jukwaani na kushika magitaa na kupiga nyimbo mbili za zamani, Africa Mokili Mobimba, na Pes Position ya OK Jazz, Komando akiliungurumisha solo mimi kwenye rythm. Kila Jumapili Mapacha huwa pale Mzalendo Millenium Tower. Mafumu Bilali Bombenga nae akatokea tukaanza stori za enziiiiiiiiiii

The Q Band kazini

Katika pita pita nikawakuta Q Band wako jukwaani pale Cine Club wakiwa chini ya Bi Leah Muddy, wakiporomosha mchanganyiko maalum wa vibao. Kwenye drums alikuweko Kejeli Mfaume mmoja wa wanamuziki waanzilishi wa Tancut Almasi Orchestra, Still going strong!!!!


The African Stars wana Twanga Pepeta Leaders Club

Kila Jumapili mchana wapenzi wa Twanga Pepeta hukusanyika Leaders Club kufaidi utamu wa muziki wa bendi yao African Stars. Nami nilikuweko Jumapili hii


Ushirikina katika muziki

Kila Jumatatu katika gazeti la SPOTILEO huwa ninakuwa na makala ya matukio mbalimbali katika muziki, makala hii nimeipa jina la KIJIWE CHA KITIME. Wiki hii nazungumzia matukio ya ushirikina katika muziki.

-->
Uchawi katika muziki…shughuli bado inaendelea Imani ya uchawi ni utamaduni ambao umekuweko katika  jamii zote za binaadamu kwa maelfu ya miaka. Historia na maandiko ya dini mbalimbali yanatukumbusha hilo na kulilaani. Huwa inategemewa kuwa kadri maendeleo na elimu yanavyoongezeka ndio imani hiyo inavyopungua na kupotea, lakini ni wazi safari bado ni ndefu kwani ukipita katika mitaa mingi utaona vibao vikiashiria waganga wanaoweza kutibu magonjwa mbalimbali, na hata kutangaza ‘kusafisha nyota’, ‘kuondoa majini’ na kadhalika. Tasnia ya muziki kwa kuwa ni sehemu ya jamii,  haijakwepa kuguswa na tatizo hilo. Kutokana na mimi mwenyewe kufanya kazi katika bendi mbalimbali niliona na kusikia vituko vingi vilivyohusishwa na imani ya uchawi. Mara ya kwanza kuanza kuona vitimbi hi…

Kilimanjaro Band (Wana Njenje),Ab kila Jumamosi huwa Salender Bridge

Kila Jumamosi kuanzia muda wa saa nne mpaka saa kumi usiku Kilimanjaro Band huporomosha muziki pale Salender Bridge. Kuna jambao la kufurahisha katika maonyesho haya, bendi hii ilianza 1974, hivyo kwa sasa ina umri wa miaka 38. Jambo ninalosema la kufurahisha ni kuwa asilimia kubwa ya wapenzi wa Njenje hawajafikia hata umri wa bendi hiyo. Vijana wenye nusu au chini ya nusu ya umri wa bendi ndio wapenzi wakubwa ambao hukesha kila Jumamosi na bendi hii.