Sunday, February 12, 2012

Mapacha Watatu....Mzalendo Pub

Huwa napata faraja sana kuwasikiliza Mapacha Watatu. Jumapili hii nilisindikizana na Mzee wa Madongo , Komando Hamza Kalala. Tukafika Mzalendo na haraka tukapanda jukwaani na kushika magitaa na kupiga nyimbo mbili za zamani, Africa Mokili Mobimba, na Pes Position ya OK Jazz, Komando akiliungurumisha solo mimi kwenye rythm. Kila Jumapili Mapacha huwa pale Mzalendo Millenium Tower. Mafumu Bilali Bombenga nae akatokea tukaanza stori za enziiiiiiiiiii


No comments:

VIJANA WA TANZANIA HUENDA WAPI KUPUMZISHA AKILI BAADA YA SAA ZA KAZI?

AWALI HAPA PALIKUWA NA JENGO LILILOITWA  NYUMBA YA SANAA WASANII WENGI WALIKUWA WAKIFANYA KAZI ZAO HAPA, KWA SASA KILICHOBAKI JINA WASANII...