Skip to main content

Posts

Showing posts from October 13, 2011

Kumbukumbu ya Kifo cha Franco 12 Oktoba 1989

Fran├žois Luambo Luanzo Makiadi  alizaliwa 6 July 1938, katika kijiji cha Soni Bata magharibi mwa jimbo la Bas Zaire huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wakati bado mchanga wazazi wake walihamia jiji la Leopodville ambalo sasa linaitwa Kinshasa. Baba yake aliitwa Joseph Emongo alikuwa mfanyakazi wa shirika la reli wakati huo mama yake alikuwa akiuza maandazi sokoni. Alipofikia umri wa miaka saba alitengeza gitaa lake akawa analipiga kwenye genge la mama yake ili kuita wateja.. Mwanamuziki maarufu Paul Ebengo Dewayon ndie aliyegundua kipaji cha mtoto huyu na kuanza kumfundisha rasmi namna ya kupiga gitaa. Mwaka 1950 akiwa na umri mdogo wa miaka 12 alichukuliwa rasmi kama mwanamuziki wa bendi ya Watam iliyokuwa inaongozwa na Dewayon. Kipaji chake kiliwashangaza wengi hasa kwa vile alikuwa akionekana umbo lake kubwa kama gitaa analolipiga lakini akiwa analipiga kwa umakini mkubwa. Akiwa na miaka 15 alirekodi nyimbo yake ya kwanza Bolingo na ngai na Beatrice (Mapenzi yangu kwa Beatrice)…