Thursday, January 30, 2014

HISTORIA YA MAREHEMU SOUD MOHAMED TIMBO (MCD). MPIGA TUMBA WA TWANGA

Marehemu alizaliwa Mwaka 1973 mkoani Kilimanjaro. MCD alisoma katika Shule ya Msingi Mawenzi iliyopo Manispaa ya Moshi na alihitimu mwaka 1987. Alianza Masomo ya Sekondari katika Shule ya Shemsanga Korogwe Tanga kuanzia 1988-1992. Baada ya kumaliza masomo ya Sekondari alijiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo.

-Baada ya kumaliza Chuo cha Sanaa Bagamoyo, alifanya kazi katika Bendi ya Diamond Sound "Wana Dar es salaam Ikibinda Nkoi", African Stars Band "Twanga Pepeta", Mashujaa Musica kwa muda mfupi na baadae alirejea katika Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" mpaka mauti yalipomfika.

-MCD alifunga ndoa na Bi Renada 2001 pia alifunga ndoa na Mwantum Zowo ambaye alikuwa dansa wa Twanga Pepeta na kwa sasa marehemu.

-Marehemu ameacha watoto wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili.

-MCD alikuwa ni kijana mcheshi, mpole na kipenzi cha watu msikivu kwa wakubwa na wadogo. Pia alikuwa mwanamuziki mahiri katika upigaji wa Ngoma (Tumba) kwa umahiri mkubwa hakuna mfano wake, ameacha pengo kubwa sana katika Bendi yake ya Twanga Pepeta.

-MCD aliugua kwa muda mfupi na kufariki usiku wa tarehe 27-01-2014 katika Hospitali ya rufaa ya KCMC.

-Familia inatoa shukrani za dhati kabisa toka Mwajiri(Twanga Pepeta), Ndugu, Jamaa na marafiki walioungana pamoja nasi tangu tulipopata msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu Soud Mohammed MCD.

MWENYEZI TUNAKUOMBA UILAZE ROHO YA MAREHEMU SOUD MOHAMMED SAID TIMBO (MCD) MAHALI PEMA PEPONI- AMEN.

SIMON MWAKIFWAMBA NA JOHN KITIME WAKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MADANSA


Simon Mwakifwamba Rais  wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) na
John Kitime Mwenyekiti wa Tanzania Musicians Network)(TMN) siku ya Jumatano walikuwa na kikao kirefu na viongozi wa juu wa Tanzania Dancers Association (TDA). Mkutano huo uliokuwa umepangwa na viongozi wa TDA ulikuwa na madhumuni ya kupata experience ya uongozi wa vyama kutoka kwa viongozi hawa ambao wamekuwa wakiongoza vyama kwa muda mrefu. Pamoja na mengine yaliyoongelewa lilikuweko swala kubwa la kuhakiki kuwa TDA wairudie Katiba yao na kuifanyia marekibisho makubwa. Jambo ambalo viongozi wa TDA waliona walipangie  ratiba na kupata msaada kutooka kwa viongozi hao wawili.
TDA ni chama kipya cha madansa ambacho kinashirikisha kila aina ya madansa, tayari kuna matawi ya Mkoa na  wilaya tatu za Dar es salaam.
KIKAO CHA TATHMINI YA TANZANIA MUSIC AWARDS 2013 CHAFANYIKA BASATA


Tanzania Music Awards 2013, leo ilifanyiwa tathmini katika ukumbi wa BASATA. Muwakilishi wa katibu Mtendaji wa BASATA, Mama Shaluwa ndie aliye kuwa Mwenyekiti wa kikao hiki cha kufanya tathmini. Wajumbe mbalimbali walikuwemo katika kikao hiki wakiwemo watangazaji wanamuziki watendaji wa BASATA, Meneja wa brand ya Kilimanjaro Premium Lager, na wawakilishi wa kampuni ya Executive Solutions. Tathmini ilianza kwa Bwana George Kavishe kutoa taarifa ya mafanikio na changamoto mbalimbali zilizokuwepo katika kuendesha  TMA 2013, na ndipo michango mingi ya kuboresha Tuzo hizi ilitolewa.  TBL iliahidi kuboresha tuzo hizi kuanzia upande wa utafutaji wa nyimbo, kuboresha utafutaji wa washiriki wa Academy na utafutaji wa Majaji. Inategemewa kuwa TMA 2014 itakuwa bora zaidi mwaka huu.