Tanzania Music Awards 2013, leo ilifanyiwa tathmini katika
ukumbi wa BASATA. Muwakilishi wa katibu Mtendaji wa BASATA, Mama Shaluwa ndie
aliye kuwa Mwenyekiti wa kikao hiki cha kufanya tathmini. Wajumbe mbalimbali
walikuwemo katika kikao hiki wakiwemo watangazaji wanamuziki watendaji wa
BASATA, Meneja wa brand ya Kilimanjaro Premium Lager, na wawakilishi wa kampuni ya
Executive Solutions. Tathmini ilianza kwa Bwana George Kavishe kutoa taarifa ya
mafanikio na changamoto mbalimbali zilizokuwepo katika kuendesha TMA 2013, na ndipo michango mingi ya
kuboresha Tuzo hizi ilitolewa. TBL
iliahidi kuboresha tuzo hizi kuanzia upande wa utafutaji wa nyimbo, kuboresha
utafutaji wa washiriki wa Academy na utafutaji wa Majaji. Inategemewa kuwa TMA
2014 itakuwa bora zaidi mwaka huu.
Comments