Skip to main content

Posts

Showing posts from September 28, 2012

TANZANIA LIVE MUSIC FESTIVAL BEGINS WITH HIGH HOPES

Mbegu mpya imepandwa leo katika anga za muziki ‘live’ Tanzania. Kwa mara ya kwanza kabisa Tamasha la muziki lililoprwa jina la Tanzania Live Music Festival limeingia anagani na kuonyesha kuwa Tanzania ina weza na ina nafasi ya aina hii ya Tamasha. Tamasha hili lililotayarishwa na Edge Entertainment ambalo litadumu kwa siku mbili na kupandisha jukwaani zaidi ya bendi kumi na mbili, lilitegemea kupata gedha ambazo zingesaidia kutunisha mfuko wa CHAMUDATA ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na pia kuupa nafasi inaostahili muziki wa dansi Tanzania.. Kama alivyosema taxi driver wa taxi iliyonirudisha nyumbani kuwa kwa mwendo huu muziki wa dansi utarudi hewani. Waliopanda jukwaani kwanza walikuwa ni Msondo Ngoma Music Band, ambao walifungua dimba kwa kupiga vibao kadhaa ambavyo kati yao viliimbwa na mkongwe mzee Gurumo. Kisha wakapanda vijana machachari wa Mashujaa Musica, waliofuatiliwa na FM Academia , ilikuwa raha tupu. Waliofuata kupanda jukwaani walikuwa ni kundi zima la Mashauz…