Skip to main content

Posts

Showing posts from February 24, 2013

Taarifa--MWANA FA-featuring Kilimanjaro Band, Mandojo na Domokaya

Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya.
Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) ungeanza kuuzwa kupitia njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za mkononi.
Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani. Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.
Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa vipengele tofauti ndani ya mi…

MISIBA YA WASANII YAIANDAMA NIGERIA

Msimu wa misiba unayoikumba tasnia ya burudani nchini Nigeria unaendelea. Baada ya msiba wa Mzee Enebeli Elebuwa, aliyefariki katika hospitali huko India tarehe 5 Desemba 2012 na kuzikwa January 11 2013, kukafuatia kifo cha mwanamuziki Goldie wiki chache zilizopita, wiki iliyopita Jumatano 20 February Mzee Justus Esiri amefariki katika hospitali baada ya kupata matatizo yaliyotokana na kuwa na kisukari. Esiri alikuwa na miaka 71, alizaliwa November 20, 1942.Umaarufu wa Esiri ulianza miaka ya 70 kutokana na tamthiliya maarufu vya Nigerian Televion Authority iliyoitwa The Village Headmaster, ambapo yeye alikuwa ndie mwalimu mkuu katika tamthiliya hiyo. Marehemu Esiri akiwa na mkewe Omiete walizaa watoto sita, mmoja wao aliyekuwa daktari wa meno aliacha fani hiyo na kuingia katika muziki na anajulikana kama Dr SID. Mungu Amlaze pema Amen