Skip to main content

Posts

Showing posts from December 6, 2012

BONGOFLEVA NA BEAT ZA KINAIJERIA

-->
Katika siku za karibuni wanamuziki kadhaa wa Tanzania wamekuwa wakija na nyimbo mpya wakiiga ‘beat’ za kutoka Nijeria. Ningependa kuwapa taarifa fupi kuhusu 'beat' hizo. Katika nchi za Afrika Magharibi, hasa Ghana na Nigeria, kwa miaka mingi walikuwa na mtindo wao wa Highlife ambao vijana wa huko wameuendeleza na kuwa mtindo ambao unatamba sana Afrika, na si mara moja wamerudia nyimbo za zamani na kutikisa Afrika,wimbo kamaSawa saware ambao uliandikwa na Rex Lawson mzee wa Kinaijeria aliyefariki mwaka 1971, ni wimbo ambao mzee huyo alianza kuupiga miaka 50 iliyopita, umechukuliwa na vijana na kupewa umri mpya kwa kuuboresha bila kuuharibu, au ukiusikiliza wimbo Sweet Mother wa Prince Nico Mbarga ambao ulitikisa Afrika kwa kufanya mauzo ya zaidi ya santurimilioni 13, utakuta pia vijana wa Kinaijeria wamechukua utaalamu wa mapigo hayo na kuja na mtindo unaotikisa Afrika. Ushauri wangu ni kuwapa hamasa vijana wanamuziki wa Tanzania kuwa kuna ghala limejaa 'beat …