Monday, October 10, 2011

Bongo Star Search yafikia fainali 14 Oktoba

Mkurugenzi wa Benchmark Productions Ritha Paulsen ametangaza rasmi kuwa finali ya BSS Second Chance itakuwa tarehe 14 October 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Katika finali hizo ambazo zitapambwa na msanii kutoka Nigeria N’ABANIA au maarufu kama MR FLAVOUR, wanamuziki wanne waliobakia watashindana na mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shilingi milioni 40, mshindi wa pili milioni 10, na watatu milioni 5.
Watakaoshindana ni Waziri Salum(BSS23), Rogers Lucas(BSS27), Bela Kombo(BSS05) na Hadji Ramadhani(BSS11).
BLOG HII INAWATAKIA KILA LA HERI WASHINDANI WOTE

Ngoma Africa wanatesa Ghana


The Ngoma Africa Band, bendi toka Tanzanian yenye makao  Ujerumani inaongozwa na mwanamuziki machachari Ebrahim Makunja aka Ras Ebby Makunja, kwa sasa iko Ghana.
The Ngoma Africa band imejipatia jina katika matamasha mbalimbali na  kwa kupitia mtindo wao wa "Bongo Dance" wamekuwa wanawatia kichaa wapenzi wa muziki kila waendapo. Nyimbo zao nyingi ni za Kiswahili na bendi inawanamuziki wakali kama mpiga solo Christian Bakotessa aka Chris-B, wengine ni Said "Jazbo" Vuai,Severn Okomo, Maxime Vayituma, Willy Mbiya, Bedi Beraca, Prince Zongolo

Ngoma Africa band imepewa jina la "The Golden Voice Of Africa"  ukitaka kusikia ngoma zao fungua www.ngoma-africa.com au www.facebook.com/ngomaafrica

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...