Sunday, June 12, 2011

Mark Band

Mark Band si jina ambalo utalikuta likizungumzwa kwenye magazeti na vyombo vyetu vya habari, kikubwa kwa kuwa wanamuziki wake si watu wenye makeke, ni watulivu na ni mara chache kuonekana katika kumbi za kawaida kama Mango au DDC Kariakoo. Lakini ni kati ya makundi yenye wanamuziki makini makini katika nchi hii. Bendi hii ambayo kila Jumatano jioni huwa pale Sea Cliff Hotel Masaki na kila Jumapili kuanzia saa kumi na moja pia huwa katika hoteli hiyo ni raha kuwasikiliza.


Drums, Sadi Majivu

Alex Senkamba, Solo Guitar

Noel Msuya Vocals

Keyboards, Jackson


Sax Rashid Pembe, Trumpet Said Makelele


K-Mondo wazee wa kibajaji

Siku za Jumapili Dar es Salaam huwa kunaendelea kuwaka moto kimuziki. Jumapili hii pale Giraffe Ocean View Hotel, palikwa raha tupu kwa hawa jamaa wakiporomosha muziki kutoka kona mbalimbali za dunia. Kila Ijumaa jioni ndo utawakuta makao yao makuu Tritz Motel Mbezi.