Skip to main content

Posts

Showing posts from August 13, 2011

Mambo Afrika Band

Mambo Afrika Band in bendi ya watu wawili ambao hutumia muziki wa sequencer katika kutoa burudani, nao si wengine bali ni Kadet Bongoman na Tabu Mambosasa, niliwakuta wakiwa katika hotel ya Concord maeneo ya Kariakoo. Ilikuwa rahaaa. Tabu kama ilivyo kwa Kadet walianza muziki kama wacheza show kwa sasa ni waimbaji mahiri sana

PFJ International Band Band ya wanamuziki ndugu

Katika pita pita  mitaani nimekutana na bendi mpya yenye mambo mapyaaa. 
Maeneo ya Sinza Mori karibu na petrol station ya Big Bon katika bar inaitwa Advantage Center nimekuta bendi ikifanya mazoezi makali, lakini bendi hii inatofauti na bendi nyingine, ni bendi ambayo idadi kubwa ya wanamuziki ni ndugu. Jina la band hii mpya ni PFJ International Band….PJF ni kifupi cha Peter Fred na Joseph. 


Joseph Kanuti- Anapiga solo, rhythm na bezi gitaa kasha pitia bendi nyingi sana kati ya hizo ni Mingomase Band iliyokuwa inaongozwa na mwanamuziki Kabatele, Tacosode Bnad, Bantu Group MCA International, DDC Mlimani Park Orchestra(Sikinde), Double M Sound, African Stars Band(Twanga Pepeta),African Minofu Band(Sumu ya Mamba),Almasi Band.

Peter Kanuti-anapiga rythm na solo gitaa, amepitia bendi zifuatazo, Bantu Group,Vijana Jazz, bendi ya Saida Karoli, Manchester Band