Friday, April 25, 2014

WANAMUZIKI 50 KUSHIRIKI KATIA UZINDUZI WA WIMBO WA MIAKA 50 YA MUUNGANO

Wanamuziki 50 kutoka aina mbalimbali za muziki watashiriki katika sherhe za miaka 50 ya Muungano na hapohapo kuzindua wimbo wa miaka 50 ya Muungano.......... Jana Alhamisi kundi hilo lilishinda Uwanja wa Taifa likifanya reharsal za wimbo huo utakao wekwa hadharani mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, na wageni waalikwa na maelfu ya watakaohudhuria sherehe hizo, na pia kurushwa katika luninga mbalimbali zitakazorusha matangazo hayo laiv. Picha za chini wasanii wakiwa katika shughuli mbalimbali uwanjani hapo.

WASANII KADHAA WA FILAMU WATUA UINGEREZA

KATIKA kile kinachoashiria ukuaji wa tasnia ya sanaa nchini wasanii kadhaa wametua Uingereza wiki hii.
Mona Lisa, Cloud, Riyama na Wastara kwa wakati huu wako London Uingereza. Mpoki akiwa Ujerumani........

MPOKI UJERUMANI......

Msanii maarufu nchini Tanzania, Muarabu wa Dubai (a k a Mpoki), ametua katika Jiji la Frankfurt na kuelekea moja kwa moja katika jiji la maraha Aschaffenburg ambapo atalala usiku mmoja na kuendelea na safari siku ya pili  kuelekea   Berlin  ambapo atahudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa watanzania Ujerumani (U T U), Kongamano la biashara pamoja na sherehe za Muungano wa Tanzania.

Mpoki alitua  katika uwanja wa kimataifa  wa Frankfurt mnamo saa 10:30 alasiri na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines akitokea Dar es salaam kupitia Addis Ababa. Msanii huyo alipokelewa na mwenyekiti wa Watanzania nchini Ujerumani.


Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...