Monday, April 25, 2011

Wanamuziki wa Tanzania nje-Ngoma Afrika Band


Ngoma Africa aka FFU, ni bendi ya Kitanzania iliyo na makao makuu Ujerumani. Bendi hii inapiga mtindo wa Bongo Dance ambao ni mchanganyiko wa muziki wa kiasili wa Kitanzania na rumba. Kiongozi wa bendi hii inayoimba nyimbo zake kwa Kiswahili ni Ibrahim Makunja au Ras Makunja. Bendi hii ilianza mwaka 1993 wanamuziki wake ni pamoja na Christian Bakotessa aka Chris B, Said Vuai aka Prince Jazbo, Maxime Buanda , Willy Mbiya na Madam Severn Onkomo . Bendi imeshatoa album kadhaa na imeshashiriki katika matamasha mengi ya muziki Ulaya. Kwa habari, muziki  na picha zaidi za bendi hii BONYA  HAPA