Saturday, May 17, 2014

ADAM KWAMBIANA HATUNAE TENA

MSANII maarufu wa filamu Adam Kwambiana  amefariki ghafla asubuhi hii, kuna hadithi tofauti kuhusu chanzo cha kifo mpaka sasa, wengine wakisema aliumwa tumbo na kuzidiwa na wengine wakisema alifariki kwa kuanguka ghafla wakati akifokeana na msanii mwenzie. Alipelekwa hospitali ya Mamam Ngoma, hatimae mwili umepelekwa Muhimbili. Adam alikuwa pia producer wa filamu, Director na muigizaji. Adam ameacha pengo kubwa katika tasnia ya filamu..
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI ADAM

IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...